📰 Newspapers

Ruto apewa miezi sita kurekebisha idara 7 alizoanzisha, ambazo sasa zimefutwa na korti

Ruto apewa miezi sita kurekebisha idara 7 alizoanzisha, ambazo sasa zimefutwa na korti

RAIS William Ruto amepewa miezi sita kurekebisha mchakato wa kuanzisha idara saba mpya za serikali baada ya Mahakama Kuu kutangaza kuwa uamuzi wa kuziunda ulikiuka Katiba na sheria.

Jaji Roselyne Aburili alibatilisha uamuzi wa Rais wa Machi 2025 ulioongeza idara za serikali kutoka 51 hadi 57, katika kipindi cha kuundwa kwa serikali jumuishi kufuatia makubaliano ya kisiasa kati yake na aliyekuwa Waziri Mkuu marehemu Raila Odinga.

Hata hivyo, jaji huyo alisimamisha utekelezaji wa uamuzi huo kwa miezi sita kuanzia Novemba 26, ili serikali iweze kufuata utaratibu unaotakiwa.

Isipofanya hivyo, agizo la kubatilisha kuundwa kwa idara hizo litaanza kutekelezwa moja kwa moja.

Idara hizo ni Usimamizi wa Uwekezaji na Mali za Umma, Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Haki na Masuala ya Katiba, Sayansi na Utafiti, Usafiri wa Anga, Mipango Maalum na Huduma za Ustawi wa Watoto.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Francis Njoroge Machi 22, 2025, akisema serikali haikushirikisha wananchi kabla ya kuanzisha idara hizo, kama inavyotakiwa na Katiba.

Jaji Aburili alisema Rais ana mamlaka ya kupanga muundo wa serikali, lakini lazima afuate masharti ya kisheria, yakiwemo kushirikisha Tume ya Utumishi wa Umma (PSC).

Mahakama ilisema serikali haikutoa ushahidi kuwa tume hiyo ilihusika katika mchakato huo au kuwa wananchi walipata nafasi ya kutoa maoni kabla ya idara kuundwa.

In brief

RAIS William Ruto amepewa miezi sita kurekebisha mchakato wa kuanzisha idara saba mpya za serikali baada ya Mahakama Kuu kutangaza kuwa uamuzi wa kuziunda ulikiuka Katiba na sheria. Kesi hiyo iliwasilishwa na Francis Njoroge Machi 22, 2025, akisema serikali haikushirikisha wananchi kabla ya kuanzisha idara hizo, kama inavyotakiwa na Katiba. Mahakama ilisema serikali haikutoa ushahidi kuwa tume hiyo ilihusika katika mchakato huo au kuwa wananchi walipata nafasi ya kutoa maoni kabla ya idara kuundwa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.